Waamurishaji wa Nafsi

ENTJ-A / ENTJ-T

Waamurishaji ENTJ-A / ENTJ-T

Una muda mfupi, kwa hivyo usiupoteze ukiishi maisha ya mtu mwingine. Usizuiwe na masharti – ambayo ni kuishi na matokeo ya fikra za watu wengine. Usiruhusu kelele za maoni ya watu wengine yazamishe sauti yako ya ndani. Na la muhimu zaidi, kuwa na ujasiri wa kufuata moyo na hisia zako. Kwa namna fulani tayari zinajua unachotaka kuwa. Kila kitu kingine kinakuja baadaye.

Steve Jobs

Waamurishaji ni viongozi wa kuzaliwa. Watu wenye aina hii ya nafsi huwa na vipaji vya karama na kujiamini, na kutoa mamlaka kwa namna inayoleta umati wa watu pamoja kufanikisha lengo moja. Lakini mbali na wenzao Wahusika Wakuu wenye hisia, Waamurishaji wanabainishwa na kiwango cha juu cha urazini, wakitumia msukumo wao, azimio na werevu kutimiza malengo yote waliyopanga kutumiza. Labda ni vizuri kwamba wanajumuisha asilimia tatu tu katika idadi ya watu, wasije wakawalemea aina oga na zenye hisia zaidi za nafsi zinazojumuisha idadi kubwa duniani – lakini tunafaa kuwashukuru Waamurishaji kwa biashara na taasisi nyingi tunazopuuza katika maisha yetu ya kila siku.

Furaha Iko Katika Shangwe ya Mafanikio

Ikiwa kuna jambo lolote ambalo Waamurishaji wanapenda, ni changamoto nzuri, kubwa au ndogo, na wanaamini kabisa kwamba wakipewa muda na rasilimali za kutosha, wanaweza kutimiza lengo lolote. Sifa hii huwafanya watu wenye aina ya nafsi ya Waamurishaji wajasiriamali wazuri, na uwezo wao wa kufikiria kimkakati na kuwa na lengo la muda mrefu huku wakitekeleza kila hatua iliyo kwenye mipango yao kwa azimio na usahihi huwafanya kuwa viongozi maarufu wa biashara. Azimio hili mara nyingi huwa utabiri wa kujitosheleza, kwa sababu Waamurishaji hufukuzia malengo yao kwa utashi kamili ambapo watu wengine wanaweza kufa moyo na kuendelea na mambo mengine, na ujuzi wao wa kijamii unamaanisha kuna uwezekano wa kuwavuta watu wote wengine pamoja nao, wakitimiza matokeo mazuri katika utaratibu huo.

Waamurishaji (ENTJ) wa Nafsi

Katika majadiliano, iwe ni katika mazingira ya kishirika au wananunua gari, Waamurishaji huwa wanaongoza, wakiwa bila huruma wala msamaha. Hii sio kwa sababu hawana huruma au ni waovu – ni kwa sababu nafsi za Waamurishaji kwa kweli hufurahia changamoto, ushindani wa akili, malumbano yanayokuja na mazingira haya, na ikiwa upande huo mwingine hauwezi kushindana, hiyo sio sababu ya Waamurishaji kukubali malengo yao ya ushindi wao wa mwisho.

Fikra msingi katika mawazo ya Muamurishaji zinaweza kuwa kitu kama “Sijali kama utaniita mwa*****amu asiye na hisia , bora ninaendelea kuwa mwa*****amu mfanisi”.

Ikiwa kuna mtu yeyote ambaye Waamurishaji wanamheshimu, ni mtu anayeweza kukabiliana nao kifikra, ambaye anaweza kutenda kwa usahihi na ubora sawia na wao. Nafsi za Muamurishaji zina ujuzi fulani wa kubainisha vipaji vya watu wengine, na kisha kusaidia katika juhudi zao za kuunda timu (kwa sababu hakuna mtu mmoja, bila kujali vipaji vyake, anaweza kufanya kila kitu peke yao), na ili kuwazuia Waamurishaji kuonyesha kiburi na uradhi. Hata hivyo, pia wana ujuzi fulani wa kutaja kasoro za watu wengine kwa kiwango cha juu bila hisia, na hapa ndipo Waamurishaji huanza kuingia mashakani.

Ukuzaji wa Sayansi ya Uhusiano na Binadamu

Kujieleza kimhemuko sio sifa kubwa kwa aina yoyote ya nafsi katika kundi la Wajibu wa Uchambuzi, lakini kwa sababu ya tabia zao za kijamii, kujitenga kwa Waamurishaji kutoka kwa mihemuko yao huwa kwa umma, na husikika moja kwa moja na idadi kubwa ya watu. Hasa katika mazingira ya kitaalamu, Waamurishaji watavunja hisia za wanaodhani kuwa sio fanisi, wasio hodari au wazembe. Kwa watu wenye aina ya nafsi ya Muamurishaji, kuonyesha muhemuko ni kuonyesha udhaifu, na ni rahisi kupata maadui ukitumia mtazamo huu – Waamurishaji watafanya vizuri kukumbuka kwamba wanategemea kuwa na timu inayofanya kazi vizuri, sio kutimiza malengo yao tu, lakini kwa uhalalishaji wao na maoni pia, jambo ambalo Waamurishaji, kwa kushangaza, huwa na hisia kuhusu.

Waamurishaji huwa na nguvu nyingi, na hubuni taswira ya kuwa wakubwa kuliko maisha – na mara nyingi huwa hivyo. Lakini watu wenye aina hii ya nafsi wanahitaji kukumbuka, kwamba hadhi zao hazipatikani kutokana na hatua zao wenyewe tu, lakini kutoka kwa hatua za timu inayowasifu, na kwamba ni muhimu kutambua michago, vipaji na mahitaji, hasa kutoka kwa mtazamo wa kimhemuko, au mtandao wao wa usaidizi. Hata kama wanafaa kukubali dhana ya “kudanganya hadi ufaulu”, ikiwa nafsi za Waamurishaji zinaweza kuchanganya lengo bora la kimuhemuko pamoja na uwezo wao mwingi, watatuzwa na uhusiano mzuri wa kuridhisha na mafanikio yote ya changamoto wanayoweza kushughulikia.

Makamanda Maarufu