“Waburudishaji” wa Nafsi

(ESFP-A / ESFP-T)

Mimi ni mchoyo, sina subira na nina uhaba kiasi wa usalama. Huwa ninafanya makosa, siambiliki na wakati mwingine mgumu kutawalika. Lakini kama huwezi kunivumilia wakati wangu mbaya zaidi, basi hunifai wakati wangu mzuri.

Marilyn Monroe

Ikiwa kuna mtu yeyote anayeweza kupatikana akiimba na kucheza densi kwa wakati mmoja, ni aina hii ya nafsi ya Waburudishaji. Waburudishaji hujikuta katika furaha za wakati wa sasa, na hutaka watu wote wahisi hivyo pia. Hakuna aina nyingine ya nafsi huwa wakarimu na muda na nguvu zao kama Waburudishaji inapokuja kuwahamasisha watu wengine, na hakuna aina nyingine ya nafsi hufanya hivyo kwa urahisi.

“Waburudishaji” wa Nafsi (ESFP-A / ESFP-T)

Sisi Sote Ni Nyota...

Wakiwa waburudishaji wa kuzaliwa, Waburudishaji hupenda kuwa kivutia hadhira, na jukwaa la dunia nzima. Watu wengi maarufu wenye aina hii ya nafsi ya Waburudishaji ni waigaji, lakini wanapenda kuwaburudisha marafiki wao pia, wakizungumza kwa umaizi wa kipekee, wakivutia watu wote na kufanya kila matembezi ya nje kuwa kama sherehe. Wakipenda kuingiliana kijamii kabisa, Waburudishaji hufurahia vitu rahisi kabisa, na hakuna furaha kubwa zaidi kwao kuliko kuwa na furaha na kundi la marafiki.

Na sio kuzungumza tu – Waburudishaji wana hisia kali sana ya ujumi kuliko aina yoyote ya nafsi. Kuanzia kujipamba, mavazi hadi makazi yanayopendeza, Waburudishaji wanapenda mitindo. Wakiwa wanajua kinachopendeza wanapokiona, Waburudishaji hawaogopi kubadilisha mazingira yao kuonyesha mtindo wao wa kibinafsi. Waburudishaji ni wadadisi wa kuzaliwa, wakichunguza miundo na mitindo mipya kwa urahisi.

Ingawa huenda ikaonekana hivyo, Waburudishaji wanajua kwamba mambo yote hayawahusu wao peke yao – huwa watazamaji, na wenye hisia kwa mihemuko ya watu wengine. Mara nyingi watu wenye nafsi hii huwa wa kwanza kusaidia mtu kuzungumzia kuhusu tatizo gumu, wakiwa tayari kutoa usaidizi wa kimhemuko na ushauri muhimu. Hata hivyo, ikiwa tatizo hili linawahusu, Waburudishaji wana uwezekano mkubwa kuepuka mgogoro badala ya kuutatua moja kwa moja. Nafsi za Waburudishaji hupenda vituko na shauku kiasi, lakini sio sana wakati wao ndiyo walengwa wa shutuma inayoweza kusababisha.

...Na Tunastahili Kumeremeta

Changamoto kubwa inayowakumba Waburudishaji ni kwamba mara nyingi huwa wanatafuta raha za haraka hadi wanatekeleza wajibu na majukumu yanayowezesha starehe hizo. Uchambuzi mgumu, kazi za marudio, na kusawazisha takwimu na matokeo halisi sio shughuli rahisi kwa watu wenye aina hii ya nafsi ya Waburudishaji. Afadhali wategemee bahati au fursa, au waombe usaidizi kutoka kwa marafiki wao wengine. Ni muhimu kwa Waburudishaji wajitahidi kufuatilia mambo ya muda mrefu kama vile mipango yao ya kustaafu au matumizi ya sukari – sio wakati wote watakuwa na mtu wa kuwasaidia kufuatilia mambo haya.

Nafsi za Waburudishaji hutambua thamani na vitu vya hali ya juu, sifa ambazo yenyewe ni nzuri. Lakini ikijumuishwa na tabia yao ya kutokuwa na mipango mizuri, sifa hii inaweza kuwafanya kuishi maisha yenye gharama kupindukia, na kadi za mikopo hasa ni hatari. Kwa kufuatilia fursa zaidi kuliko kupanga malengo ya muda mrefu, Waburudishaji wanaweza kugundua kwamba kutokuwa makini kumefanya mambo mengine kuwa ghali kuyamudu.

Hakuna kitu kinachomfanya mtu mwenye aina hii ya nafsi ya Waburudishaji kukosa furaha kama kugundua kwamba wamezuiwa na hali fulani, na kushindwa kujiunga na marafiki wao.

Waburudishaji hukaribishwa mahali popote panapohitaji ucheshi, utani, na mtu wa kujitolea kujaribu jambo lipya na la kufurahisha – na hakuna furaha kubwa kwa nafsi za Waburudishaji kuliko kuwafurahisha watu wote. Waburudishaji wanaweza kupiga gumzo kwa saa nyingi, wakati mwingine kuhusu kitu chochote mbali na mada waliyotaka kuzungumzia, na kushiriki mihemuko ya wapendwa wakati mzuri na mbaya. Ikiwa wanaweza kukumbuka kupanga mambo yao, watakuwa tayari kujihusisha katika mambo yote mapya na ya kufurahisha yaliyomo duniani, pamoja na marafiki wao.

Waburudishaji Ambao Huenda Ukawa Unawajua

Ungependa kujifunza zaidi?