Mtetezi
Wachukulie watu kana kwamba wako vile wanapaswa kuwa, na hivyo utawasaidia kufikia uwezo wao halisi.
Watu wenye nafsi ya INFJ (Watetezi) ni wenye maadili na malengo makubwa – hawatosheki tu kupita maisha bila kugusa mabadiliko, wanataka kusimama kidete na kuleta utofauti. Kwa watu hawa wenye huruma, mafanikio hayapimwi kwa pesa au hadhi bali kwa kutafuta utimilifu wa ndani, kuwasaidia wengine, na kuwa nguvu ya wema duniani.
Ingawa wana malengo na matarajio makubwa, INFJs hawapaswi kuonekana kama “waotaji wasiofanya kazi.” Watu wenye aina hii ya nafsi wanajali sana uadilifu, na huwa hawaridhiki hadi wapate kufanya walichoamini kuwa sahihi. Wakiwa waangalifu sana, husonga maishani wakiwa na ufahamu mkali wa maadili yao, wakiwa makini kutoacha kamwe kile kilicho cha muhimu – siyo kulingana na watu wengine au jamii, bali kulingana na hekima na uchunguzi wao wenyewe.
Kutafuta Kusudi
Labda kwa sababu aina hii ya nafsi ni nadra sana, INFJs mara nyingi hubeba hisia – iwe wanazitambua au la – kwamba wako tofauti na watu wengi. Kutokana na maisha yao ya ndani yaliyo tajiri na hamu yao ya dhati ya kutafuta makusudi maishani, hawapati urahisi kufanana na wanaowazunguka. Hii haimaanishi kwamba INFJs hawawezi kufurahia kukubalika au kuwa na mahusiano ya karibu – ni kwamba wakati mwingine hujiona wamekosolewa au hawana maelewano na ulimwengu unaowazunguka.
Kwa bahati nzuri, hisia hii ya “kutokuwa sambamba na wengine” haiathiri ahadi ya INFJs ya kutaka kuufanya ulimwengu uwe mahali bora zaidi. Nafsi hizi huchukizwa sana na dhuluma, na mara nyingi huweka umuhimu zaidi kwenye ukarimu kuliko maslahi yao binafsi. Mara nyingi hujiona wameitwa kutumia uwezo wao – ikiwemo ubunifu, fikra za kufikirika, na hisia – kuinua wengine na kusambaza huruma.
Watu wengi wenye nafsi ya INFJ wanaona kuwasaidia wengine kama wito wao, na huendelea kusaka fursa za kuingilia kati na kutetea kilicho sahihi. Watu wenye aina hii ya nafsi pia hutamani kurekebisha matatizo makubwa ya jamii, wakiwa na matumaini kwamba dhuluma na ugumu wa maisha vitabaki historia. Hata hivyo, wakati mwingine INFJs wanaweza kuweka akili zao sana kwenye ndoto zao kiasi cha kusahau kujitunza ipasavyo – jambo linaloweza kusababisha msongo wa mawazo na kuchoka kupita kiasi.
Kuungana na Wengine (na Kujitambua Wenyewe)
INFJs wanathamini mahusiano ya kina na halisi na wengine. Ni mambo machache sana yanayowapa furaha kama kumfahamu mtu mwingine kwa upana – na kufahamika vivyo hivyo. INFJs hufurahia mazungumzo yenye maana kuliko kupiga stori juu juu, na huwa na namna ya kujieleza iliyo ya joto na hisia. Uaminifu na uwazi huu wa kimhemuko unaweza kuwaacha wengine wakiwa na taswira kali kabisa juu yao.
Wakiwa wasikivu na mara nyingi wasiojiwekea maslahi binafsi, INFJs huwekeza kiasi kikubwa cha nishati na kujali katika mahusiano yao, lakini hii haimaanishi kwamba wakati wote wanahisi kutambuliwa vya kutosha. Watu wenye aina hii ya nafsi hupenda kuchelewesha kila hatua na kutafakari kwa kina madhara wanayoweza kusababisha kabla ya kutenda. Kwa sababu hiyo, inaweza kuwachosha wanapoona watu wengine hawatambui nia zao njema. INFJs ni wahisivu sana kwa aina yoyote ya ukosoaji na wanaweza kuchukulia mambo binafsi kupita kiasi.
Dhamira Binafsi
INFJs wengi huamini kwamba maisha yao yana kusudi la kipekee – dhamira ambayo waliwekwa duniani kutimiza. Kwao, moja ya vipengele vyenye kuwapa kuridhika zaidi maishani ni kutafuta kusudi hili – na kisha, wakishalipata, kujitahidi kulitimiza ipasavyo.
INFJs wanapokutana na hali ya kutokuwepo kwa usawa au uonevu, mara chache sana hukata tamaa – badala yake, hutegemea uwezo wao wa muona-mbele na huruma yao ili kutafuta suluhisho. Kutokana na uwezo wao asili wa kusawazisha moyo na akili, watu hawa waliojitolea wana mwitiko wa haraka kurekebisha makosa duniani, haijalishi ni madogo au makubwa kiasi gani. Kile wanachohitaji kukumbuka ni kwamba, wanapokuwa bize kuwaangalia wengine, hawana budi pia kujipumzisha wakati fulani na kujitunza wenyewe.