“Weledi” wa Nafsi

(ISTP-A / ISTP-T)

Nilitaka kuishi maisha, maisha tofauti. Sikuwa ninataka kuenda mahali pamoja na kuona watu wale wale na kufanya kazi hiyo hiyo kila siku. Nilikuwa ninataka changamoto za kuvutia.

Harrison Ford

Weledi wanapenda kutafuta kwa mikono na macho yao, wakigusa na kuchunguza mazingira yao kwa urazini mzuri na udadisi mkali. Watu wenye nafsi ya aina hii huwa Watengenezaji wa kuzaliwa, wakihama kutoka mradi hadi mwingine, wakiunda mambo muhimu na ya ziada kwa furaha zao tu, na kujifunza kutoka kwa mazingira wanayozuru. Wengi wao wakiwa makanika na wahandisi, nafsi ya Weledi hufurahia kufanya kazi kwa mikono yao wakifungua na kufunga vitu, lakini kwa ufanisi bora kuliko walivyokuwa hapo awali.

“Weledi” wa Nafsi (ISTP-A / ISTP-T)

Weledi hupekua dhana kwa ubunifu, usuluhishaji, na majaribio na uzoefu wa mtu binafsi. Nafsi hizi hufurahia watu wengine wakivutiwa na miradi yao na wakati mwingine huwa hata hawajali watu wengine wakiingilia kazi zao. Bila shaka, hiyo ni kwa masharti kwamba watu hao wasiingilie kanuni na uhuru wa Weledi, na watahitajika kuwa wazi kwa Weledi wanapoonyesha matakwa yao kwa nia njema.

Watu wenye aina hii ya nafsi ya Weledi hufurahia kusaidia na kushiriki uzoefu wao, hasa na watu wanaowajali, na ni aibu kubwa kwamba ni wachache sana, wakijumuisha takriban asilimia tano ya idadi ya watu. Wanawake Weledi hasa ni wachache zaidi, na majukumu ya kawaida ya kijinsia ambayo jamii inatarajia huenda ikawa haziwafai – mara nyingi wataonekana kama wanawake wenye tabia za kiume kuanzia umri mchanga.

Thubutu kuwa Tofauti

Ingawa tabia yao tulivu na kufuatilia mambo halisi kunaweza kuwafanya watu hawa kuonekana kuwa rahisi kueleweka mara ya kwanza, Weledi huwa watatanishi. Wakiwa marafiki lakini wasiri sana, wapole lakini hufanya mambo kwa ghafla, wadadisi sana lakini hawawezi kuwa makini na masomo rasmi, nafsi za Weledi zinaweza kuwa ngumu kutabiri, hata kwa marafiki na wapendwa wao. Weledi wanaweza kuonekana wakiwa waaminifu sana na imara kwa muda mfupi, lakini huwa wanakusanya nguvu ya kutotulia inayojionyesha bila onyo, na kubadilisha mwelekeo wa matakwa yao upande mwingine.

Badala ya kuwa na jitihada zenye dira, Weledi hutafuta tu uwezekano wa matakwa mapya wanapofanya mabadiliko haya ya makubwa.

Maamuzi ya Weledi hutoka kwa hisia ya uhalisi wa utendaji, na katika mioyo yao kuna hisia kubwa ya usawa wa moja kwa moja, mtazamo wa “watendee watu wengine”, ambayo kwa kweli husaidia kueleza tabia nyingi za kushangaza za Weledi. Badala ya kuwa makini zaidi, wakiepuka kukera watu wengine ili kuepuka kulipiziwa kisasi, watu wenye aina hii ya nafsi ya Weledi wanaweza kufanya mambo kupindukia, wakikubali adhabu, iwe nzuri au mbaya, kama haki.

Suala kubwa zaidi ambalo nafsi za Weledi wanaweza kukumbana nalo ni kwamba mara nyingi huchukua hatua haraka sana, wakipuuza asili yao ya uhuru na wakidhania watu wengine ni sawa na wao. Watakuwa wa kwanza kusema mzaha wa kukera, kujihusisha kabisa katika mradi wa mtu mwingine, kutenda kwa makeke na kufanya utani, au kubadilisha mipango yao kwa ghafla kwa sababu kumetokea mpango mwingine unaowavutia zaidi.

Hakuna Kitu Kinachosha kama Watu Wote Kukubaliana na Wewe

Weledi watakuja kujua kwamba aina zingine nyingi za nafsi zina mipaka rasmi ya sheria na tabia zinazokubalika kuwaliko – nafsi zenye hisia nyingi mara nyingi huwa hawataki kusikia mzaha wa kukera, na bila shaka hawawezi kusema mzaha kama huo, na hawangetaka kujihusisha katika michezo ya makeke, hata na mtu anayetaka. Ikiwa kuna mhemuko, kukiuka mipaka hii kunaweza kuwa na matokeo mabaya kinyume na matarajio.

Weledi wana shida fulani ya kutabiri mihemuko, lakini ni moja ya asili zao za usawa, ikizingatia jinsi ilivyo vigumu kupima mihemuko na vichocheo vya Weledi. Hata hivyo, tabia yao ya kupekua uhusiano wao kupitia vitendo vyao badala ya kuwaelewa watu wengine inaweza kusababisha hali zingine ngumu sana. Watu wenye aina hii ya nafsi ya Weledi huwa na matatizo ya mipaka na miongozo, wakipendelea uhuru wa kuzurura na kutenda nje ya mipaka ikiwa inahitajika.

Kupata mazingira wanayoweza kufanya kazi na marafiki wazuri wanaoelewa mtindo wao na kutotabirika kwa vitendo vyao, wakijumuisha ubunifu wao, ucheshi wao na mtazamo wao wa kujifanyia mambo kutafuta suluhisho na mambo halisi, kutawapa watu Weledi miaka mingi yenye furaha ya kuunda visanduku muhimu – na kuvitamani kutoka nje.

Weledi Ambao Huenda Ukawa Unawajua

Ungependa kujifunza zaidi?