“Waongozaji” wa Nafsi

(ENFJ-A / ENFJ-T)

Kila kitu unachofanya sasa hivi kinaenea nje na kuathiri kila mtu. Mkao wako unaweza kufurahisha moyo wako au kusambaza wasiwasi. Pumzi yako inaweza kusambaza upendo au kuleta huzuni chumbani. Mtazamo wako unaweza kuzua furaha. Maneno yako yanaweza kuhamasisha uhuru. Kila kitendo unachofanya kinaweza kufungua mioyo na akili.

David Deida

Waongozaji ni viongozi wa kuzaliwa, wenye upendo na karama. Wakijumuisha asilimia mbili ya idadi ya watu, watu wenye nafsi hii mara nyingi huwa ni wanasiasa wetu, makocha wetu na walimu wetu, wanaowahamasisha watu wengine kutimiza na kufanya mambo mazuri duniani. Wakiwa na ujasiri asili unaosababisha ushawishi, Waongozaji hujivunia na kufurahia kuwaongoza watu wengine kushirikiana ili kujiimarisha wao wenyewe na kuboresha jamii zao.

“Waongozaji” wa Nafsi (ENFJ-A / ENFJ-T)

Waumini Thabiti wa Watu

Watu huvutiwa na nafsi imara, na Waongozaji husambaza uhalali, ushirika na ungwana, hawaogopi kusimama na kuzungumzia jambo wanaloona linafaa kusemwa. Uwezo wao wa kuzungumza na watu wengine huwajia kwa urahisi, hasa mazungumzo ya ana kwa ana, na sifa yao ya umaizi huwasaidia watu wenye nafsi ya Waongozaji kushawishi kila mtu, iwe kwa mambo ya kweli na mantiki au hisia tupu. Waongozaji huona motisha wa watu na matukio yanayoonekana kuwa tofauti kwa urahisi, na wanaweza kuleta dhana hizi pamoja na kuziwasilisha kama lengo moja kwa ufasaha unaovutia kabisa.

Mvuto wa Waongozaji kwa watu wengine ni wa kweli kabisa – wakati watu wenye nafsi hii wanamwamini mtu, wanajihusisha kabisa katika matatizo ya mtu huyo, na kuwaamini kabisa. Kwa bahati nzuri, imani hii huwa utabiri wa kujitimiza, kwani ungwana na ukweli wa Waongozaji unawahamasisha wanaowajali kujiimarisha wenyewe. Lakini ikiwa nafsi hizi hawatakuwa makini, wanaweza kusambaza matumaini yao kupindukia, wakati mwingine wakiwasukuma watu wengine mbali ya walipo tayari au kuwa na hiari ya kuenda.

Waongozaji wana udhaifu mwingine pia: huwa wana uwezo mkubwa wa kuangazia na kuchambua hisia zao wenye, lakini wakijiingiza kwenye matatizo ya mtu mwingine, wanaweza kuwa na unyong'onyevu wa kimhemuko, wakiona matatizo ya watu wengine yakiwa yao, wakijaribu kutatua kitu ndani yao ambacho hakina kasoro. Ikiwa watu hawa watafika mahali wanapozuiwa na mapungufu ya mtu mwingine, inaweza kuzuia uwezo wa Waongozaji kuona mbele ya mtanziko na kuwa wa manufaa yoyote. Jambo hili likifanyika, ni muhimu kwa Waongozaji kujiondoa na kutafakari hali yao ili watenganisha kati ya wanachohisi, na ni suala gani tofauti linahitaji kutatuliwa kutoka mtazamo mwingine.

...Matatizo Hayafai Kutuzuia Kuunga Mkono Jambo Tunaloamini Kuwa la Haki

Waongozaji ni watu wa kweli, watu wanaojali wanaofanya wanayosema, na hakuna kitu kinawafurahisha zaidi kuliko kuongoza, wakipatanisha na kuhamasisha timu yao kwa ari ya kuambukiza.

Watu wenye aina hii ya nafsi ya Waongozaji ni wangwana wenye shauku kabisa, na kuna uwezekano wasiogope kupigana kuwatetea watu na dhana wanazoziamini. Sio ajabu kwamba Waongozaji wengi maarufu ni viongozi wa kisiasa na kitamaduni wenye ushawishi mkubwa – aina hii ya nafsi inataka kuongoza njia ya maisha bora yajayo, iwe ni kwa kuongoza taifa kwa mafanikio, au kuongoza ligi ndogo ya timu ya softiboli hadi ushindi baada ya ushindani mkali.

Waongozaji Ambao Huenda Ukawa Unawajua

Ungependa kujifunza zaidi?